NEW YORK: Mkutano wa dharura kuhusu Lebanon
14 Julai 2006Matangazo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana kwa kikao cha dharura kulijadili suala la Lebanon.Mjumbe wa Lebanon katika Umoja wa Mataifa ameomba msaada wa kukomesha moja kwa moja mashambulio yanayofanywa na Israel.Kikao hiki kimeitishwa kuambatana na ombi lililotolewa na serikali ya Lebanon.Muda mfupi kabla ya kufunguliwa mkutano huo,makao makuu ya Hezbollah kusini mwa mji mkuu wa Lebanon,Beirut yalishambuliwa kwa mabomu na vikosi vya Kiisraeli.