1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Kuna pengo la usalama Lebanon

23 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIx

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Mashariki ya Kati ameonya kwamba itachukuwa hadi miezi mitatu kuziba kile alichokiita pengo la usalama kusini mwa Lebanon.

Terje Roed- Larsen amesema uvunjaji wa makubaliano ya kusistisha mapigano usiokusudiwa unaweza kuzusha tena mapigano kati ya Israel na Hezbollah.Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanatazamiwa kuwa na mkutano wa dharura hapo Ijumaa kujadili mchango wa wanajeshi wa Umoja wa Ulaya katika kikosi cha kulinda amani cha kimataifa nchini Lebanon.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

Vikosi vya wanajeshi wa Ulaya vinaonekana kuwa muhimu kwa Umoja wa Mataifa kuweza kupata wanajeshi wa kutangulia 3,500 kusini mwa Lebanon kufikia Septemba pili.