1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Korea Kaskazini ikatazwe kufanya jeribio la silaha za nyuklia

7 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFFm

Mkuu wa IAEA - Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa amesema,viongozi wa kimataifa wanapaswa kuishinikiza Korea ya Kaskazini kutofanya jeribio la silaha za kinyuklia.Mkurugenzi Mkuu wa IAEA,Mohamed El Baradei aliwaambia maripota katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York,kuwa matokeo ya ya kisiasa na kimazingira ya jeribio hilo yatakuwa balaa kubwa.El Baradei alikuwa akizungumza pembezoni mwa mkutano uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa kuzuia utapakaji wa silaha za kinyuklia.Amesema suala la Korea ya Kaskazini linahitaji kushughulikiwa kwa haraka,hasa kufuatia ripoti za upelelezi za hivi karibuni kuwa Pyongyang labda inajiandaa kufanya jeribio la kinyuklia.Serikali ya Marekani mjini Washington imeonya kuwa jeribio lolote la silaha za kinyuklia litakalofanywa na Korea Kaskazini ni kitendo cha uchokozi.