NEW YORK: Kilimo cha mipopi kimeongezeka Afghanistan
27 Juni 2007Matangazo
Uzalishaji wa afyuni nchini Afghanistan mwaka jana uliongezeka kwa asilimia 50.Ripoti iliyotolewa na Idara ya madawa ya kulevya na uhalifu ya Umoja wa Mataifa imesema,zaidi ya asilimia 90 ya afyuni duniani hutoka Afghanistan. Hiyo ni licha ya kuwepo msaada wa kimataifa kujaribu kuyateketeza mashamba yenye mimea ya mipopi.kwa upande mwingine,ripoti hiyo imesema, juhudi za kupambana na kilimo cha afyuni katika eneo la Asia ya Kusini-Mashariki zimefanikiwa.