1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Hatari ya kuzuka janga la kiutu Lebanon

21 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5X

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameonya juu ya hatari ya kuzuka janga kubwa la kiutu nchini Lebanon.Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa,Jan Egeland amesema,msaada wa chakula hauwezi kupelekwa kusini mwa Lebanon kwa sababu barabara na madaraja yamebomolewa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amezitaka pande zote mbili katika mgogoro huo zihakikishe kuwa msaada ulio muhimu unaweza kupelekwa.Wakati huo huo,Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa msaada wa Euro milioni 10 kwa ajili ya Lebanon.Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso amesema,msaada huo utapelekwa katika kipindi cha siku chache zijazo.Amesema,mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasio ya kiserikali yatakabidhiwa msaada huo ili yaweze kuwahudumia watu wenye shida.