NEW YORK: Azimio la Lebanon limepitishwa kwa kauli moja
12 Agosti 2006Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepitisha azimio linalotoa mwito wa kuumaliza mgogoro wa Lebanon.Kabla ya kupigwa kura,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan alilihotubia baraza hilo na akawakosoa wanachama wake kwa kukosa kuchukua hatua wakati wa mgogoro huo.Azimio lililopitishwa linataka mapigano yote yasitishwe na Israel iondoke kutoka ardhi ya Lebanon.Vile vile kikosi cha Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 15 elfu kikisaidiwa na idadi hiyo hiyo ya majeshi ya Lebanon,kitasimamia operesheni ya kuondosha majeshi ya Israel kutoka ardhi ya Lebanon.Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert pia amelikaribisha azimio hilo licha ya upinzani wa serikali yake.Olmert amezungumza na rais wa Marekani George W.Bush na ametoa shukrani kwa kuungwa mkono na Washington.