NEW YORK. Annan ataka tume ya amani nchini Sierra Leone ifutwe.
6 Mei 2005Matangazo
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Kofi Annan, anataka tume ya kulinda amani ya umoja huo nchini Sierra Leone ifutiliwe mbali kwani kuna utulivu na usalama katika taifa hilo.
Katika ripoti yake aliyoiwasilisha kwa baraza la usalama la umoja huo, Annan amependekeza wanajeshi hao waanze kuondoka nchini humo kuanzia mwezi Agosti hadi Disemba tarehe 31 mwaka huu.
Huku hali ya usalama ikiwa bado haijafikia kiwango cha kuridhisha na kwamba taifa hilo bado linahitaji msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa, hayo yanaweza kufikiwa na serikali ikishirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na mataifa mengine, na wala sio tume ya kulinda amani.