NEW YORK : Afrika yaitakia msaada Somalia
14 Agosti 2007Mataifa ya Afrika hapo jana yameushinikiza Umoja wa Mataifa kutowa msaada wa kulinda amani kwa Somalia sawa na ule uliotolewa awali kwa jimbo la Dafur nchini Sudan.
Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa Somalia ulisikiliza ombi la Umoja wa Afrika la kutaka msaada huo ulingane na mojawapo ya mipango miwili ya misaada ijulikanao kama masada mwepesi na msaada mzito iliopitsihwa kujaribu kukomesha umwagaji damu huko Dafur.
Baraza hilo limejibu kwa kutoa rasimu ya azimio yenye kutaka mipango zaidi kwa kikosi cha ziada kwa ajili ya operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa kuchukuwa nafasi ya kikosi cha Umoja wa Afrika kiliopo Somalia lakini bila ya kujifunga kwamba itatuma kikosi hicho.
Umoja wa Afrika ilipaswa kuwa na wanajeshi 8,000 nchini Somalia lakini hadi sasa ina wanajeshi 1,600 tu nchini humo kutoka Uganda.