New Orleans. Kazi ya kutafuta maiti imeanza.
10 Septemba 2005Maafisa mjini New Orleans wanalenga hivi sasa katika kuwatafuta watu waliokufa kutokana na mafuriko katika mji huo.
Hadi kazi hiyo itakapomalizika , maafisa wanasema hakutakuwa na hatua za haraka za kuwaondoa watu ambao wanakataa kuondoka katika mji huo licha ya amri iliyotolewa ya kuwaondoa kwa nguvu.
Zaidi ya watu 300 wamethibitishwa kuwa wamekufa katika jimbo la Alabama , Mississippi na Louisiana , licha ya kuwa idadi kubwa ya vifo ilitarajiwa.
Kiasi cha watu milioni wamepoteza makaazi yao kutokana na uharibifu uliosababishwa na kimbunga Katrina.
Majeshi ya Marekani ambayo yanaendelea na kazi katika eneo hilo yameanza ujenzi mpya na kurejesha huduma muhimu.
Mamia kwa maelfu ya watu wanaendelea kukosa umeme, na maji ya bomba bado si salama kunywa katika maeneo kadha.