1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI: India na Pakistan zasaini mkataba kuzuia vita vya nyuklia

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPr

India na Pakistan zimetia saini mkataba kati yao unaolenga kupunguza hatari ya kuzuka kwa bahati mbaya vita vya kinyuklia.

Mkataba huo ulisainiwa wakati wa mkutano kati ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Pakistan, Khurshid Kasuri na mwenyeji wake wa India, Pranab Mukherjee, mjini New Delhi.

India pia imeahidi kuripoti kwa Pakistan juu ya uchunguzi wa mashambulio ya mabomu dhidi ya treni ya abiria iliyowaua watu 68 na kuwajeruhi wengine wengi.

Waathiriwa wengi wa mashambulio hayo dhidi ya treni hiyo iliyokuwa njiani kwenda Lahore nchini Pakistan ikitokea New Delhi India walikuwa raia wa Pakistan.