Netanyahu: Vita vya Gaza vina gharama kubwa kwa Israel
24 Desemba 2023Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyasema hayo baada ya jeshi la Israel IDF kutangaza kwamba wanajeshi 14 wameuwawa katika ardhi ya Palestina kuanzia siku ya Ijumaa.
Katika taarifa yake, Waziri Mkuu huyo ameapa kuendelea na mapambano kwa nguvu hadi watakapofikia malengo yao ikiwemo kulitokomeza kundi la Hamas, kuwarejesha mateka na kuhakikisha Gaza si tishio tena kwa taifa la Israel.
Aidha ameweka wazi kwamba vita katika Ukanda wa Gaza itakuwa ya muda mrefu, hadi pale hali ya usalama itakaporejea katika maeneo ya Kaskazini na Kusini.
Tangu kuanza kwa mapigano hayo, jeshi la Israel limepoteza askari 153 huku pia likikabiliwa na mashambulizi mengine kutoka wanamgambo wa Hezbollah katika mpaka wake wa kaskazini na Lebanon.