MigogoroIsrael
Waziri Mkuu Netanyahu awakumbuka wahanga wa Oktoba 7
7 Oktoba 2024Matangazo
"Siku hii ya leo, kwenye eneo hili na mengineyo hapa nchini mwetu, tunawakumbuka waliouawa, mateka wetu, ambao tutahakikisha wanarudi, mashujaa wetu wa kijeshi waliokufa wakiipigania nchi yetu. Tumeshuhudia mauaji makubwa mwaka uliopita na tumesimama tena kama taifa, na kama simba," Amesema Netanyahu.
Netanyahu aliambatana na meya wa Jerusalem Moshe Lion kwenye mnara huo ulioandikwa majina ya waliouawa kwenye shambulizi hilo la Hamas lililowaua watu 1,200.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais na mgombea wa urais nchini Marekani Kamala Harris amelaani shambulizi hilo akisema kile ilichokifanya Hamas ni ushetani, ukatili na kitendo cha kuudhi na kuongeza kuwa anahuzunishwa sana na vifo na uharibifu katika eneo la Gaza.