1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaji Lubuva avitaka vyombo vya habari kuacha upendeleo

Amina Abubakar29 Septemba 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) inavilaumu vyombo vya habari kwa kuandika habari zisizo sahihi wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25, ikisema zitawakanganya wapigakura.

https://p.dw.com/p/1GfDK
Picha: Getty Images/Afp/Johannes Eisele

Bila kuvitaja kwa majina, mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, anasema vyombo hivyo vinaonekana kuegemea vyama fulani wakati wa kupeperusha matangazo yao na kuandika ripoti ambazo zinaweza kuwapa wananchi taswira isiyo sahihi na hivyo akavitaka kuwajibika katika utendaji wao. Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wa habari mkongwe na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania, Atilio Tagalile, na akitaka kujua iwapo taarifa ya NEC ina ukweli wowote. Sikiliza mazungumzo yao kwa kubonyenza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi