NEC yasema maandalizi ya uchaguzi Tanzania yaendelea vyema
18 Agosti 2020Sehemu ya maandalizi ambayo NEC imewebainishwa ni pamoja na uboreshaji wa daftari likiwa na wapiga kura 29,188,347, vituo vya kupigia kura viilivyopangwa ni 80,155 ambapo kwa Tanzania bara ikiwa na vituo 79,670 na kwa upande wa Zanzibar NEC itatumia vituo 1,412, hii ikiwakilisha idadi ya wapigakura 500 kwa kila kituo.
Soma pia Magufuli akabidhiwa cheti, Zanzibar bado si shwari
Mwenyekiti wa NEC jaji mstaafu Semistocles Kaijage amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam Jumanne, kwamba hadi sasa maandalizi yanaendelea vema, ambapo hadi siku hiyo, vyama vya siasa 16 vimeshachukua fomu ya kuomba kuwania nafasi ya urais huku vikiwa tayari vimekubaliana katika maadilizi ya uchaguzi yatakayozingatia, sheria, haki za binadamu pamoja na kutotumia maneno yuyatakayohatarisha amani ya taifa hilo.
Soma pia Uchaguzi Mkuu Tanzania Oktoba 28
Mwaliko kwa waangalizi wa kimataifa
Aidha tume hiyo imesema tayari imewasiliana na wizara inayoshughulikia mambo ya nje, kutoa mialiko kwa waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na sekretarieti ya Jumuia ya Madola ili kuwasilisha maombi ya kufanya uangalizi huku ikiundwa kamati maalum itakayoratibu masuala yote ya waangalizi wa uchaguzi huo wa tano kufanyika tangu kuundwa kwa mfumo wa vyama vingi.
Soma pia Unayopaswa kujuwa kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015
Mkurugenzi wa uchaguzi Wilson Mahera amesema tume imeandaa mwongozo utakaosimamia waangalizi hao, ikijumuisha maadili ambayo yakikiukwa hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Katika hatua nyingine ikiwa imesalia siku chache kufunguliwa kwa kampeni za uchaguzi chama cha upinzani ACT wazalendo kupitia kiiongozi wake Zito Kabwe, kimetambulisha hadharani kikosi kazi ambacho kitahusika katika kampeni za uchaguzi, kinachojumuisha watu kutoka kada mbalimbali ikiwemo sheria pamoja na siasa.
Soma pia Waziri wa zamani wa mambo ya nje kuwania urais Tanzania
Kabla ya kufunguliwa kwa kampeni wagombea watatakiwa kurejesha fomu na NEC kupitisha wagombea endapo watakuwa wamekidhi vigezo kwa mujibu wa katiba na sheria.