Matokeo yote kutangazwa vituoni
30 Septemba 2015Matangazo
Pirikapirika za kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba zinazidi kushika kasi. Taarifa ya NEC iliyosema ni ya kusimamia haki katika mchakato huo inasema kwa sasa kura zote kuanzia udiwani, ubunge na Urais zitahesabiwa katika vituo vya kupiga kura na matokeo yake kutolewa hapo hapo katika kipindi kisichozidi masaa 72.
Sudi Mnette anazungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Rutaraka Ate Junior, juu ya kauli hii ya NEC na maana yake kwa uchaguzi wa mwaka huu unaotajwa kuwa wa kihistoria.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Josephat Charo