1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndugu wawili mapacha kudhibiti madaraka nchini Poland

8 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG9a

Poland inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambapo ndugu wawili mapacha huenda wakashika hatamu za uongozi wa nchi hiyo..Waziri mkuu KAZIMIERZ MARCINKIEWICZ ameuarifu uongozi wa chama tawala cha kihafidhina-Haki na usawa uamuzi wake wa kujizulu.Nafasi yake huenda akakabidhiwa mkuu wa chama hicho Jaroslaw KACZYNSKI-ndugu pacha wa rais wa Poland.Vyombo vya habari vya Poland vilizungumzia hapo awali juu ya mvutano mkubwa kati ya waziri mkuu aliyejiuzulu MARCINKIEWICZ anaesemekana kufuata msimamo wa wastani na ndugu wawili mapacha KACZYNSKI.Mkutano kati ya MARCINKIEWICZ na kiongozi wa upande wa upinzani ndio uliozidisha makali ya mvutano kati ya waziri mkuu na kiongozi wa chama tawala.