Ndege zisizo na rubani kupambana na malaria Zanzibar
7 Novemba 2019Matangazo
Ndege hiyo isiyokuwa na rubani iliyotolewa na kampuni ya China ya DJI, ilitumika kunyunyiza madawa katika mashamba ya mpunga ambayo yamevamiwa na mbu kisiwani Zanzibar ili kuunda chanda chembamba juu ya maji.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo ya DJI, mbinu hiyo ya kunyunyiza madawa katika mashamba ya mpunga na kuunda chanda chembamba juu ya maji, itayazamisha mabuu na viluilui vya mbu na hatimaye kuviuwa. Watafiti hao wanatarajia kuwa mbinu hiyo itasaidia pakubwa kupunguza idadi ya mbu.
Ugonjwa wa Malaria huua mamia ya watu kila mwaka hasa barani Afrika. Mnamo mwaka 2017, takwimu za shirika la afya duniani WHO zilionyesha kuwa Malaria ilisababisha vifo vya watu 435,00 kote duniani.