1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ngome za waasi yashambuliwa Yemen

14 Julai 2015

Mashambulizi hayo yameendelea licha ya Umoja wa Mataifa Kutangaza mpango wa kusitishwa kwa mapigano Kati ya pande zinazozana kwa lengo la kufanikisha usambazaji misaada ya kibinadamu.

https://p.dw.com/p/1FyHq
Jemen Lulftangriff
Picha: picture-alliance/dpa/Y. Arhab

Kupitia msemaji wake Stephane Dujarric, Katibu Mkuu wa umoja huo Ban Ki Moon ameelezea kusikitishwa na hatua ya kupuuzwa kwa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini humo. Hata hivyo ameelezea matumaini kwamba makabiliano hayo yatafikia kikomo.

Huku hayo yakijiri, maafisa wa afya nchini humo wanasema takribani watu 10 wameuliwa kwenye shambulio lililotekelezwa Jumanne usiku. Hata hivyo Shirika la Habari la Saba linachomilikiwa na waasi wa Huthi linasema waliouliwa ni watu 25 na wengine 50 kujeruhiwa.

Inaripotiwa kuwa kikosi cha muungano kimeyashambulia maeneo yanayodhibitiwa na wasi wa Shia wanaoungwa mkono na Iran na washirika wake, ambao ni wanajeshi walio watiifu kwa Rais wa Taifa hilo Ali Abdullah Saleh, katika mikoa ya Aden na Lahj. Kwa mujibu wa aliyeshuhudiwa, shambulio hilo lililenga jengo la kijeshi la uhandishi katika mji wa Saawana viungani kwa mji mkuu Sanaa.

Zubereitung von Nahrung auf Feuerstellt im Jemen
Hali ya kiutu nchini Yemen inazidi kuwa mbayaPicha: DW/M. al-Haidari

Eneo la kusini, wapiganaji walifanikiwa kuwarejesha nyuma waasi katika eneo la Ras Amran Magharibi ya Aden. Watu 17 waliwamo waasi waliaga dunia. Jana Jumatatu, kikosi cha muungano kilidhibiti barabara kuu karibu la Al-Waht, kilomita 15 Kaskazini mwa Aden huku waasi 10 na wapiganaji 12 watiifu kwa Hadi wakiuawa.

Mashambulizi hayo yameendelea licha kipindi cha siku sita cha kusitishwa kwa mapigano kilichotangazwa na Umoja wa Mataifa, kilichoanza kutekelezwa Ijumaa usiku wa manane. Waasi wa Kishia wanasema hawajapokezwa rasmiombi la kusitisha mapiagnoi hayo, huku kiongozi wa waasi wa Huthi akisema hakutarajia kutekelezwa kwa agizo hilo la Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema Bw Ban hajakata tamaa na angali anasisitiza haja ya kuzingatiwa kwa agizo hilo pasi na vikwazo. Amesisitiza pia kwamba mjumbe wa umoja huo nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed alikuwa ameeleza haja ya kuchukuliwa hatua hiyo kutokana na hali ilivyo nchini humo.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni 21.1, ambao ni zaidi ya asilimia 80 ya raia nchini humo wanahitaji msaada, huku watu 3,200 wakiwa wamefariki duniani tangu mwezi Machi mwaka huu.

Mwandhishi: Geoffrey Mung'ou
Mhariri: Mohamed Abdul'Rahman