SiasaChina
Ndege za kivita za China zaingia eneo la kijeshi la Taiwan
8 Juni 2023Matangazo
Msemaji wa wizara ya ulinzi mjini Taipei Sun Li-Fang amesema ndege za China zimeanza kuingia katika eneo la ulinzi la Taiwan saa kumi na moja alfajir, na kwamba zoezi hilo limehusisha ndege 37. Msemaji huyo ameongeza kuwa baadhi ya ndege hizo zimeendelea hadi magharibi mwa bahari ya Pasifiki kuendelea na luteka za upelelezi.
Wizara ya ulinzi ya kisiwa hicho ambacho China inadai ni himaya yake, imesema imeendelea kuifuatilia kwa makini hali hiyo, na kwamba iliweka tayari meli na ndege zake na kuyaweka makombora katika hali ya tahadhari.