Ndege za Kijeshi nchini Kenya zashika doria mpakani mwa Somalia
4 Juni 2008Matangazo
Ndege hizo zinashika doria karibu na eneo la Liboi ambako wapiganaji wa Somalia walishambulia kituo kimoja cha polisi mwishoni mwa juma lililopita.Kwa mujibu wa wakaazi wa eneo hilo shambulio hilo lilifanywa na kundi lijulikanalo kama Shabaab ambalo Marekani imeliweka kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.
Ili kupata picha halisi katika eneo hilo la mpaka Thelma Mwadzaya amezungumza na Bogita Ongeri afisa wa uhusiano katika Wizara ya Ulinzi nchini Kenya.