Nchi 23 za Umoja wa Ulaya zimechukua hatua kuelekea muungano wa kijeshi, ambao zinaamini utaimarisha mshikamano baada ya uamuzi wa Uingereza kujiondoa katika umoja huo. Muungano huo utajulikana kama PESCO, kifupi cha maneno ya Kiingereza ambayo maana yake ni Muundo wa Kudumu kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Ulinzi.