Nchi za G7 zasisitiza kuendelea kuiunga mkono Ukraine
17 Novemba 2024Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye ni mwenyekiti wa kundi la G7 mwaka huu, ameihakikishia Ukraine kuhusu uungwaji mkono usioyumbayumba wa mataifa hayo.
Viongozi wa Marekani, Canada, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italia na Japan wamesema Urusi bado ni kizuizi pekee cha amani ya kudumu. Wamesema Urusi itaendelea kukabiliwa na vikwazo na udhibiti wa mauzo ya nje kutoka kwenye nchi za Magharibi na washirika wake.
Soma Pia: Viongozi wa G7 kujadili uhamiaji, Afrika na akili mnemba
Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi yake ingependa kuvimaliza vita mwaka ujao kwa njia za kidiplomasia. Maoni yake ni kutokana na kutokuwa na uhakika juu ya mwelekeo wa baadaye wa vita hivyo.
Rais wa mteule wa Marekani, Donald Trump, ameapa kusitisha mapigano atakapoingia madarakani mwezi Januari. Siku ya Jumanne, Ukraine itaadhimisha siku 1000 tangu Urusi ilipoivamia.