Nchi tano zapata viti Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
4 Januari 2023Matangazo
Balozi wa Msumbiji Pedro Comissario Afonso, ameiita kuwa siku ya kihistoria, huku Balozi wa Uswisi Pascale Baeriswyl, akisema anajisikia kuwa mwenye unyenyekevu na wajibu, wakati nchi zao zilianza mihula yao ya kwanza kabisa, kwenye taasisi hiyo yenye nguvu zaidi ya Umoja wa Mataifa.
Msumbuji ilichukua nafasi ya Kenya ambayo ilimaliza muhula wake.
Malta imejiunga kwa mara ya pili, Equador mara ya nne na Japan kwa mara ya 12. China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani ndio wajumbe wa kudumu wenye kura ya turufu kwenye baraza hilo.