1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi kadhaa zaorodheshwa kumulikwa kwa utakatishaji wa fedha

24 Juni 2023

Shirika la kimataifa la kupambana na uhalifu wa kuwekeza fedha haramu, FATF limeziweka Cameroon, Croatia na Vietnam kwenye orodha yake ya kuzifuatilia kwa karibu nchi hizo.

https://p.dw.com/p/4T1Ey
LOGO FATF

Tamko hilo limetolewa siku ya mwisho ya mkutano wa wanachama 39 wa FATF uliofanyika mjini Paris, Ufaransa. Nchi hizo tatu zinaungana na nyingine 23 katika juhudi za kuyashughulikia mapungufu ya serikali zao katika mikakati ya kukabiliana na utakatishaji fedha.

Nchi hizo zinashirikiana kikamilifu na shirika la FATF linalopambana na uhalifu wa kutakatisha fedha, ufadhili wa ugaidi na kuongezeka kwa ufadhili haramu wa fedha. Baraza hilo limezigawa nchi kwenye orodha mbili ya kijivu ambayo nchi husika hufuatiliwa kwa karibu na nyeusi ambayo huyahusisha mataifa yaliyo kwenye hatari kubwa.

Iran, Myanmar na Korea Kaskazini ni nchi zilizo pia kwenye orodha hiyo ambapo zinachunguzwa. Zaidi ya nchi 200 zimekubali kutekeleza viwango vya shirika la FATF. Mapendekezo ya shirika hilo ni pamoja na hatua zinazohusu uwazi, kuratibisha njia za kuzuia uhalifu na kutoa adhabu.