Nchi 40 zaitaka China kuheshimu haki za binaadamu
7 Oktoba 2020Matangazo
Balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa, Christoph Heusgen amesema wanaitaka China kuheshimu haki za binaadamu hasa za makabila ya watu wachache pamoja na dini, kwenye majimbo ya Xinjiang na Tibet. Miongoni mwa nchi 38 zilizosaini wito huo ni pamoja na Marekani na nchi nyingi za Umoja wa Ulaya ikiwemo Albania na Bosnia, pamoja na Canada, Haiti, Hondurus, Japan, Australia na New Zealand. Nchi hizo pia zimeelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya Hong Kong. Hata hivyo, balozi wa Pakistan alisimama na kusoma taarifa iliyosainiwa na nchi 55 ikiwemo China, inayolaani unafiki wa nchi zinazoitumia hali ya Hong Kong kama kisingizio cha kuingilia masuala ya ndani ya China.