NATO yatiwa hasara tena.
9 Oktoba 2010ISLAMBAD:
Malori ya mafuta takriban 30 ya majeshi ya Nato yameshambuliwa nchini Pakistan.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi shambulio hilo lilifanyika katika jimbo la Baluchistan kusini magharibi mwa Pakistan. Msafara huo wa malori ulikuwa upeleke mahitaji kwa ajili ya majeshi ya kimataifa yaliyopo nchini Afghanistan.
Majeshi ya Nato yanalazimika kutumia njia ya kusini magharibi mwa Pakistan kwa sababu Pakistan imeifunga njia iliyopo kwenye mpaka wake muhimu kufuatia mkwaruzano na Marekani
Polisi wawili pia walijeruhiwa katika shambuli hilo.Taarifa ya serikali imesema kwamba washambuliaji wapatao 10 walitumia bunduki na roketi kuyateketeza malori hayo ya kusafirishia mafuta yaliyokuwa yameegeshwa njiani karibu na mkahawa.
Shambulio hilo nila sita kufanyika mnamo muda wa wiki moja.