NATO yatakiwa iwalipe fidia familia za wahanga wa mashambulio
28 Oktoba 2006Matangazo
Shirika la haki za binaadam Human Rights Watch limeitaka jumuia ya kujihami ya magharibi NATO iwalipe fidia familia za wahanga wa mashambulio ya hivi karibuni nchini Afghanistan.Human Rights Watch linaikosoa tume ya umoja wa mataifa inayoongozwa na NATO -ISAF kwa kutofanya chochote kuwalinda wananchi wa Afghanistan.Jumuia ya kujihami ya magharibi NATO imekiri jana,watu 12 wameuwawa kufuatia mashambulio ya hivi karibuni kusini mwa Afghanistan.Katibu mkuu wa jumuia ya NATO Jaap de Hoop Scheffer ameomba radhi kama alivyosema “kwa msiba huo.”Wakati huo huo mkuu wa wanamgambo wa Taliban Mullah Omar amelikataa pendekezo la rais Hamid Karzai la kuitishwa mazungumzo ya amani nchini Afghanistan.