NATO yashindwa kuidhinisha mpango mpya wa ulinzi
16 Juni 2023Matangazo
Mwanadiplomasia mmoja ameilaumu Uturuki kwa kukosekana kwa maelewano hayo. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema mawaziri hao waliangazia upya mipango hiyo, hiyo ikiwa mara ya kwanza tangu mwisho wa Vita Baridi, hatua iliyochochewa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Stoltenberg awali alisema kwamba mawaziri hao wanakaribia kuelewana. Hatua hiyo inaashiria mabadiliko makubwa ya kimsimamo kwa NATO kwa kuwa jumuiya hiyo awali ilikuwa haioni haja ya kuwa na mipango mikubwa ya kujilinda, kwa kuwa ilikuwa inapigana vita vidogo nchini Afghanistan na Irak na ilihisi kwamba Urusi haina kitisho chochote baada ya utawala ule wa Umoja wa Sovieti.