1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yakubali kuondoa majeshi Afghanistan 2014

20 Novemba 2010

Ingawa NATO imetoa ratiba hiyo ya 2014 kumaliza operesheni za kijeshi, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani asema wao bado hawajaamua.

https://p.dw.com/p/QEOa
Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen akiwa LisbonPicha: AP

Rais wa Urusi Dmitry Medvedev amewasili mjini Lisbon, Ureno kwa mazungumzo kuhusiana na mfumo wa ulinzi wa pamoja wa makombora ya kujihami pamoja na mkakati wa vita nchini Afghanistan. Huu ndio mkutano wa kwanza kati ya Jumuiya ya Mataifa ya Magharibi NATO na Urusi katika miaka miwili. Mapema viongozi wa Jumuiya hiyo wanaohudhuria mkutano huo wa siku mbili walikubaliana kuanza kuyaondoa majeshi yao Afghanistan kuanzia mwaka ujao, lakini wakaapa kwamba hawatoiacha serikali ya Afghanistan kulemewa na kundi la Taliban ambalo bado ni kitisho. Mataifa hayo 48 ambayo yana majeshi yao Afghanistan walisaini mkataba na rais Hamid Karzai kuyapa majeshi ya Afghanistan jukumu la usalama wa nchi yao kuanzia mwaka ujao 2011 na kuondoka kabisa 2014. Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen alisema Jumuiya hiyo bado itaiunga mkono Afghanistan hata baada ya kumalizika rasmi kwa opereshini za mapigano.

NATO Gipfel Portugal Lissabon November 2010
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan.Picha: AP