NATO yaidhinisha mkakati mpya wa ulinzi
22 Novemba 2010Matangazo
Katika mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la Kujihami la NATO uliofanyika mjini Lisbon, Ureno, viongozi hao wameidhinisha mpango mpya wa miaka 10 ijayo unaoliruhusu Shirika hilo kupambana na vitisho vipya vya ugaidi.
Hii ni pamoja na uvamizi wa mitandao. Mipango ya kuunda mfumo wa pamoja wa ulinzi na Urusi, pia ilijadiliwa. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameutaja mkutano huo wa NATO kama nafasi muhimu katika uhusiano kati ya mataifa ya Mashariki na Magharibi. Hii ni mara ya kwanza kwa Urusi kushiriki katika mkutano huo wa NATO.
Mwandishi: Maryam Abdalla/DPAE, Reuters
Mhariri: Sekione Kitojo