SiasaUbelgiji
NATO yaapa kuiunga mkono Ukraine bila kuchoka
24 Februari 2023Matangazo
Katika taarifa yake iliyoitoa ikiwa ni mwaka mmoja baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, NATO imesema Urusi inapaswa kusitisha vita vyake haramu, ambavyo vinaathiri utaratibu wa usambazaji wa chakula na nishati ulimwenguni na kuitaka Moscow kuwajibika kutokana na uhalifu wake wa kivita.
Kadhalika tamko hilo pia limewajumuisha wanaoiwezesha Urusi katika vita hivyo vilivyogharimu maisha ya maelfu ya raia, wengine wakikimbia taifa hilo, ikiwa ni pamoja na Belarus na Iran ambayo iliipatia Urusi ndege zisizokuwa na rubani aina ya Shaheed.