SiasaKosovo
NATO kutuma wanajeshi 700 zaidi Kosovo, kukabili maandamano
31 Mei 2023Matangazo
Tayari walinda amani 30 wamejeruhiwa katika vurugu hizo. Vurugu hizo zilitokea kuanzia wiki iliyopita baada ya mameya wa kabila la Albania waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliosusiwa na Waserbia, walipojaribu kuingia ofisini. Wakati Waserbia walipowazuia, polisi ya Kosovo ilirusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji. Marekani na Umoja wa Ulaya zimeongeza juhudi zao za upatanishi kati ya Serbia na Kosovo wakihofia kukosekana kwa utulivu katika eneo hilo hasa wakati huu ambapo vita vingali vinaendelea nchini Ukraine.