NATO KUTOA MAFUNZO KWA JESHI LA IRAQ
22 Februari 2005Matangazo
BRUSSELS:
Shirika la ulinzi la magharibi-NATO limeahidiwa na wanachama wake wote 26 kuwa watachangia aina fulani ya mafunzo na zana kwa wanajeshi wa Iraq.
Afisa aliearifu hayo ambae hakutaka kutajwa jina alisema jumla ya nchi 15 zimeahidi kutuma maafisa wa kutoa mafunzo ya kijeshi mjini Baghdad.Nchi nyengine pamoja nazo Ufaransa na Ujerumani-zilizopinga vita vya Iraq,zimejitolea kutoa mafunzo nje ya Iraq au kugharimia kifedha .