1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kutangaza usitishaji mashambulio nchini Libya wiki ijayo

Sekione Kitojo22 Oktoba 2011

Jumuiya ya NATO imesema kuwa ina mpango wa kusitisha ujumbe wa kijeshi wa kushambulia maeneo nchini Libya yaliyodumu miezi saba, ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, siku moja baada ya kuuwawa Muammar Gaddafi

https://p.dw.com/p/12wpi
Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen.Picha: dapd

Jumuiya ya NATO imesema kuwa ina mpango wa kusitisha mashambulio yake ya anga na baharini yaliyodumu miezi saba chini Libya, ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, siku moja baada ya kifo cha kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi. Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema jana kuwa uamuzi huo ni wa awali na utatangazwa rasmi mapema wiki ijayo. Ameongeza kuwa anajisikia fahari kwa kile jumuiya hiyo ilichofanikisha pamoja na washirika wake katika hujuma hizo.

Wakati huo huo mzozo kuhusiana na taratibu za mazishi ya mwili wa Gaddafi umechelewesha kuzikwa kwake. Taratibu za dini ya Kiislamu zinataka mwili wa marehemu kuzikwa haraka iwezekanavyo, lakini viongozi katika baraza la mpito la taifa wanasema kuwa mazingira yaliyosababisha kifo chake siku ya Alhamis, ni lazima yajulikane. Waziri mkuu wa mpito amesema kuwa Gaddafi ameuwawa katika mapambano ya silaha baina ya wale wanaomuunga mkono na wapiganaji wa serikali. Lakini picha za video za kukamatwa kwake zimesababisha watu wengi kuamini kuwa alipigwa risasi mara tu baada ya kukamatwa.