NATO kuondoka Libya 31 Oktoba
28 Oktoba 2011Maafisa wa shirika la kujihami la NATO wanatarajiwa kukutana mjini Brussels Ubelgiji hii leo (28.10.11), kutangaza rasmi mwisho wa operesheni yake ya vita vya angani vya miezi 7 nchini Libya.
Katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen hapo jana amesema NATO ipo tayari kuusaidia utawala mpya katika kuingia kwenye demokrasia pekee, lakini hakuna jukumu la ziada kwa shirika hilo nchini Libya, na hii inatoa nafasi ya kumalizika operesheni ya NATO mwishoni mwa mwezi huu.
Mashambulio ya NATO yalichangia pakubwa katika kuondolewa madarakani utawala wa kiongozi wa zamani Muammer Gaddafi.
Hatahivyo utawala wa mpito Libya umeiomba NATO kuendeleza kampeni yake hadi mwishoni mwa mwaka huu ukisema kuwa wafuasi wa Gaddafi bado ni kitisho kwa nchi hiyo.
Mwandishi: Maryam Abdalla/alle