NATO, G7 kuendelea kuibeba Ukraine
13 Julai 2023Viongozi wa kundi la mataifa tajiri duniani, G7, na wale wa Umoja wa Ulaya wametangaza mpango wa kimataifa wa kuendelea kuisaidia Ukraine kijeshi na kuipatia uwezo mkubwa wa kuweza kujilinda na kujihami.
Mpango huo wa kuisaidia Ukraine utajumuisha vifaa na mafunzo ya kijeshi, kubadilishana taarifa za kijasusi, na teknolojia ya ulinzi wa mtandaoni.
Soma zaidi: Mkutano wa NATO: G7 yatoa ahadi kwa Ukraine
G7 kutangaza mpango wa muda mrefu wa usalama kwa Ukraine
Rais Joe Biden wa Marekani amesema G7 itaisaidia Ukraine kuimarisha jeshi lake wakati ikisubiri kujiunga na NATO.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema hapo jana kuwa mkutano huo wa NATO unaonesha kuwa muungano huo wa kijeshi unarejea kwenye mikakati ya Vita Baridi, na kwamba Urusi itakuwa tayari kujibu vitisho kwa wakati muafaka na kwa njia inayofaa, kwa kutumia mifumo na mbinu zote walizonazo.