Nassiriya, Iraq: Waziri wa ulinzi wa Italia azuru Iraq
13 Novemba 2003Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Italia Antonio Martino, leo ameelekea katika mji wa kusini mwa Iraqi kuwazuru askari wa kitaliani waliojeruhiwa katika shambulizi la kujitolea muhanga maisha, ambamo watu 27 waliuawa, pamoja na Wataliani 18. Msemaji wa Italia Andrea Angeli, aliliambia shirika la habari la Reuters, kwamba Martino alipowasili tu, alikwena moja kwa moja hospital na anatarajiwa pia kukagua kituo cha mripuko wa jana, katika makao ya polisi wa jeshi mkabala na mto Euphrates. Mripuko huo ulibomoa jengo la kangriti la ghorofa tatu, ukawaua polisi 16 Wataliani na raia wawili wa Italia, kiwango kikubwa kabisa cha vifo vya wanajeshi wa Italia katika shambulizi moja tangu vita vya pili vya dunia.