Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA, umeahirisa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wake uliokuwa ufanyike leo kuanzia saa moja usiku. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari muungano huo umesema kuwa, umechukua hatua hiyo ili kuwapa wafuasi wake kwenye dini ya kiislamu kukamilisha mfungo wao.