1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAPLES / ITALIA: Bunge la nchi za ulaya na eneo la mediteranianlaanzishwa

2 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvt
Wakuu wa Bunge la Ulaya, na wenzao kutoka nchi za kaskazini mwa bara la Afrika, wameanzisha bunge la ulaya na eneo la Mediteranian.

Habari kuhusu kuanzishwa bunge hilo, zimetangazwa na mwenyekiti wa Bunge la ulaya Bwana Pat Cox, pamoja na mwenyekiti wa baraza la wawakilishi nchini Moroco, Bwana Abdelwahad Radi, kandoni mwa mkutano unaofanyika katika mji wa Italy Naples, wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za jumuia ya Umoja wa Ulaya, na wenzao wa nchi za eneo la Mediteranian-

Viongozi hao wawili wamesema bunge hilo litakuwa na wabunge miambili arbaine. Miamoja ishirini watakua kutoka nchi za bara la Ulaya na Jumuia ya Umoja wa Ulaya, na wengine miamoja ishirini watakua wabunge kutoka nchi za eneo la mediteranian, ambazo si za bara la ulaya-

Duru za kidiplomasia mjini Naples zimearifu uamuzi kuhusu makao makuu ya bunge hilo bado haujachukuliwa, lakini tayari inafikiriwa miji miwili; mji wa Italy Naples, pamoja na mji wa Misri Alexandria-