Nani anapambana kwenye vita vya Syria?
Vita vya raia nchini Syria vilizuka baada ya vuguvugu la mageuzi la Waarabu lililogubika Mashariki ya Kati na Afrika Magharibi mwaka 2011. Mzozo huo tangu wakati huo umehusisha makundi yanayohasimiana duniani kote.
Syria: Kitovu cha mzozo
Syria imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2011, baada ya rais wa Syria, Bashar al-Assad kupoteza udhibiti wa eneo kubwa la nchi hiyo yaliyochukuliwa na makundi ya kimapinduzi. Mzozo huo tangu kuanza kwake umehusisha mataifa ya nje na kusababisha taabu na vifo vya raia wengi.
Dikteta
Jeshi la Syria, linalotambulika rasmi Syrian Arab Army (SAA), linamtii rais wa Syria Bashar al-Assad na linapigana kurejesha mamlaka ya rais nchini humo. SAA limekuwa likipambana kwa kushirikiana na idadi kubwa ya wapiganaji wanaomuunga mkono Assad, ambao ni pamoja na jeshi la kitaifa, NDF na kushirikiana na washauri wa kijeshi wa Urusi, wanaomuunga mkono rais Assad.
Waasi
Kikosi cha Free Syrian Army kilitokana na waandamanaji waliopinga utawala wa Assad, na kwa hatua lilipata nguvu. likishirikiana na makundi mengine yasiyo ya jihadi, lilitaka kuondoshwa rais Bashar al Assad na uchaguzi wa kidemokrasia. Baada ya kuangushwa mara kadhaa, wengi wa wafuasi wake walijiunga na makundi ya kigaidi. Liliungwa mkono na Marekani na Uturuki, lakini nguvu yake imepunguzwa sana.
Upinzani
Mapambano kati ya Wakurdi wa Syria na makundi ya Kiislamu katika eneo la kaskazini na magharibi mwa Syria ni mzozo wa kujitegemea. Kundi la kikabila waliojazana Uturuki, Syria na Iraq, Wakurdi kwa muda mrefu wametaka kuwa na uhuru wao ndani ya nchi zao. Uturuki inawachukulia wapiganaji wa Kikurdi ndani ya mipaka yake kuwa ni magaidi.
Wapiganaji wapya wa jihadi
"Dola la Kiislamu" (IS) ilitumia mwanya wa machafuko ya kikanda kuchukua eneo kubwa nchini Iraqi na Syria mwaka 2014. Wakati ikitaka kuanzisha eneo lake la utawala, "IS imekuwa na sifa mbaya kutokana na chapa yake ya imani kali ya dini ya Kiislamu na mauaji ya watu wengi. IS inakabiliwa na anguko baada ya majeshi yanayoongozwa tofauti na Marekani na Urusi kuwakabili wapiganaji hao.
Majihadi wa zamani
IS sio kundi pekee la kigaidi lililofanya uharibifu Syria. Makundi mengine ya wapiganaji wa Kiislamu kama al- Nusra Front lenye mahusiano na al-Qaeda-linked linalojulikana pia kama Jabhat Fatah al-Sham, wanapigana kwenye mzozo huo. Wakipigana wao kwa wao, dhidi ya Assad na waasi wa msimamo wa wastani, al-Nusra Front limejiunganisha na vyombo vingine chini ya mwamvuli wenye jina Tahrir al-Sham.
Msaidizi wa Mashariki
Ikulu ya Urusi, Kremlin, imethibitika kuwa rafiki mwenye nguvu wa Rais Assad. Majeshi ya ardhini ya Urusi yalijiunga rasmi kwenye mapigano Septemba 2015 baada ya miaka kadhaa ya kusaidia jeshi la Syria. Moscow ilikosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa kwa idadi kubwa ya vifo vya raia kutokana na mashambulizi ya angani iliyofanya.
Washirika wa Magharibi
Marekani na mataifa mengine ya NATO yalikataa kutuma majeshi ya ardhini kusaidia katika mzozo wa Syria, lakini yalimpinga Assad na kuwaunga mkono waasi wa msimamo wa wastani. Muungano unaoongozwa na Marekani wa takriban nchi 60, ambazo ni pamoja na Ujerumani, ulianza kuwalenga IS na magaidi wengine kwa mashambulizi kutoka angani, mwishoni mwa mwaka 2014.
Mlinzi wa Kaskazini
Uturuki ambayo pia ni sehemu ya majeshi yanayoongozwa na Marekani dhidi ya IS, kwa kiasi kikubwa imewaunga mkono waasi wa msimamo wa wastani wanaompinga Assad. Ina uhusiano mzuri na washirika wa Marekani, hata hivyo kuhusu mashirikiano ya Marekani na wapiganaji wa Kikurdi, baadhi yao wanawaunga mkono Wakurdi wanaotaka kujitenga ndani ya Uturuki.
Kivuli cha Kiajemi
Iran ilimuunga mkono rais wa Syria, Bashar al-Assad kabla ya mzozo wa sasa. Huku ikiwa na nia ya kuendeleza ushawishi wake Mashariki ya Kati, Tehran imeisaidia Damascus tangu mwaka 2011 kwa mikakati, mafunzo ya kijeshi na majeshi ya ardhini. Kwa kuwa inamsaidia Assad na kushirikiana na Urusi, Iran iko kama adui ambaye si wa moja kwa moja wa Marekani nchini Syria.