NANCY UFARANSA:Kansela Schroeder awataka wafaransa waikubali katiba mpya ya Umoja
20 Mei 2005Matangazo
Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder amewatolea mwito wananchi wa Ufaransa waikubali katiba mpya ya Umoja wa ulaya pindi itakapopigiwa kura ya maoni mnamo wiki ijayo.
Kansela Schroeder ametoa mwito huo alipokutana na marais Jacque Chirac wa Ufaransa na rais Alesander Kwasniewski wa Poland mjini Nancy Ufaransa.
Hata hivyo kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kuna mgawanyiko miongoni mwa wafaransa juu ya suala la katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.
Bunge la Ubelgiji limeipitisha katiba hiyo ambayo itapelekwa katika mabunge ya mikoa ili kuidhinishwa.
Tayari katiba hiyo imekubaliwa na mataifa saba ya Umoja wa Ulaya.