1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nana Akufo- Addo aapishwa kuwa rais wa mpya wa Ghana

7 Januari 2017

Nana Akufo- Addo ameapishwa leo kuwa rais wa mpya wa Ghana. Akufo-Addo ameahidi kupunguza kodi ili kufufua uchumi wa nchi hiyo kando na kuangamiza ufisadi serikalini

https://p.dw.com/p/2VSCN
Afrika Ghana - Nana Akufo-Addo übernimmt das Amt des Präsidenten
Picha: Reuters/L. Gnago

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 72, na ambaye ni wakili wa zamani wa kutetea haki za binadamu, alichukua kiapo cha ofisi katika hafla iliyoandaliwa leo kwenye uwanja wa uhuru jijini Accra na kuhudhuriwa na wageni 6,000 na umati mkubwa.

Rais huyo mpya amesema ni lazima kurejesha uadilifu serikalini, na kwamba fedha za umma hazipaswi kutumika visivyo na chama kinachoshinda uchaguzi bali kukuza rasrimali za nchi na maendeleo kiuchumi. Na kwa watu waliomchagua, rais Akufo Addo alikuwa na Ujumbe huu.

Wakuu wa nchi 11 walihudhuria sherehe hiyo akiwemo mtangulizi wake anayeondoka madarakani John Dramani Mahama. Nana Akufo-Addo alimshinda John Mahama katika uchaguzi wa rais mwezi jana, naye Mahama akakubali kushindwa, hali ambayo imeifanya Ghana kutajwa kama mhimili imara wa demokrasia katika eneo hilo.