Namibia yaongeza hali ya tahadhari kufuatia ujangili wa faru
2 Aprili 2024Matangazo
Wizara ya mazingira katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imeeleza kuwa kumeitishwa mkutano wa dharura wa ngazi ya juu na maafisa wa usalama ili kupanga mikakati ya kukabiliana na wimbi la ujangili wa kikatili.
Mwaka 2022, faru 87 waliuawa kote nchini Namibia na takwimu za mwaka jana bado hazijatolewa.
Soma zaidi: Twiga katika hatari ya kutoweka
Mwishoni mwa mwaka huo wa 2022, kulikuwa na wastani wa faru 23,300 barani Afrika, na takriban faru 15,000 wanapatikana nchini Afrika Kusini.
Pembe za faruhung`olewa baada ya kuuawa na majangili ambao huziuza katika masoko ya barani Asia wanakozitumia katika madawa ya kienyeji.