Namibia yafuta sheria za marufuku kwa mapenzi ya jinsia moja
21 Juni 2024Matangazo
Jumuiya inayotetea haki za jamii ya wapenzi wa jinsia moja katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imeutaja uamuzi huo kuwa wa kihistoria, ambao utatokomeza ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja waliokuwa wakiishi kwa hofu ya kukamatwa.
Soma zaidi: Sheria ya kupinga LGBTQ nchini Iraq yakosolewa na wanaharakati
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanaharakati Friedel Dausab kwa usaidizi wa shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Uingereza la Human Dignity Trust.
Karibu nusu ya nchi 54 za Afrika zimepiga marufuku mapenzi ya jinsia moja.
Afrika Kusini ni nchi pekee barani Afrika inayoruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja na kuwapa haki ya kuasili watoto.