1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Waandishi wa habari wa Somalia wakwama mpakani

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTC

Chama cha wanahabari wa Somalia kimetoa mwito kwa ulimwengu uwasaidie waandishi wa habari wa Somalia wanaotoroka hali mbaya ya usalama mjini Mogadishu na waruhusiwe kuvuka mpaka kati ya Somalia na Kenya.

Chama cha waandishi habari wa Somalia kimetoa taarifa kwamba hali mbaya ya usalama iliyopo mjini Mogadishu imewalazimu takriban waaandishi habari 30 kutoroka na kutafuta hifadhi nchini Kenya.

Waandishi kumi wa habari kutoka Somalia wamekwama mpakani wakisubiri ruhusa ya kuingia mkoa wa kaskazini mashariki nchini Kenya kutokana na vizuizi vilivyowekwa kwenye mpaka huo na kuanzishwa agizo la visa kabla ya kuvuka na kuingia Kenya kwa raia wote wote wa Kisomali.

Katibu mkuu wa chama cha waandishi wa habari wa Somalia Faruk Osman ameitaka serikali ya mpito ya Somalia iingilie kati na wakati huo huo ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa itoe misaada ya kibinadamu kwa waandishi hao wa habari.