1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Viongozi wa kanisa Anglikana barani Afrika watofautiana juu ya mwito wa wenzao wa Marekani kuhusu Ushoga

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMO

Viongozi wa kanisa la Kianglikana barani Afrika wanatofautiana katika maoni juu ya mwito uliotolewa na Askofu wa kanisa hilo nchini Marekani wa kutaka paweko hali ya kuvumiliana na kuepusha mifarakano ya kidini katika suala la kuidhinishwa askofu mwingine ambaye anajihusisha na vitendo vya kufanya ngono na watu wa jinsia moja.

Msemaji wa kanisa Anglikana nchini Uganda Aron Mwesigye amesema amefurahishwa na mwito huo wa Askofu huyo wa Marekani lakini nchini Kenya Kasisi Stephen Njihia Mwangi ametilia shaka mwito huo akisema umetolewa katika muda usiofaa kwa kuwa zimesalia siku chache kabla ya siku ya mwisho jumapili ijayo ambapo viongozi wa kanisa hilo Afrika walikuwa wameitenga kwa wenzao wa Marekani kuahidi kutomtawaza askofu mwingine Shoga au kuidhinisha misa rasmi za wasenge na wasagaji.