NAIROBI:Safari za ndege kwenda Somalia kuondolewa vikwazo
24 Julai 2007Matangazo
Kenya inapanga kuondoa baadhji ya vikwazo vya safari za ndege hadi nchini Somalia.Vikwazo hivyo viliwekwa miezi tisa iliyopita baada ya Marekani kuonya kuwa wanamgambo wa kisomali wanapanga mashambulizi nchini Kenya na Ethiopia.Wapiganaji wa Mahakama za kiislamu walioteka mji wa Mogadishu wakati huo walifurushwa Disemba mwaka jana lakini wapiganaji wanaoaminika kuhusika na kundi hilo bado wanaendelea na mashambulizi.
Wapiganaji hao wanataka nchi ya Somalia ifuate sheria za kiislamu.Baadhi ya tahadhari mpya zilizowekwa ni kufanyiwa ukaguzi wa ndege kila zinapofika mjini Wajir nchini Kenya kwasababu za usalama kabla ya kuendelea na safari zake nchini Somalia.