1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Mkutano wa kimataifa juu ya hali ya hewa waendelea Nairobi

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvI

Mkutano wa kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa unaendelea mjini Nairobi nchini Kenya.Mkutano huo uliofunguliwa hapo jana utajadili kuhusu njia za kupunguza hali ya ujoto duniani baada ya rasimu ya kyoto kumalizika muda wake hapo mwaka 2012.

Akifungua mkutano wa jana makamu war ais wa Kenya bwana Moody Awori alielezea ongezeko la ujoto duniani kama ni kitisho kikubwa ambacho hakijapata kumkabili mwanadamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa iliyotolewa kabla ya mkutano wa jana, mabadiliko ya hali ya hewa yataangamiza sehemu nyingi za bara la Afrika kufuatia kuendelea kuongezeka kwa kiwango cha joto.