Nairobi. Wanarakati wapinzani wa utandawazi waandamana.
21 Januari 2007Maelfu ya wanaharakati wapinzani wa utandawazi walifanya maandamano katika eneo kubwa masikini kabisa katika bara la Afrika jana Jumamosi kuadhimisha mwanzo wa mkutano wa dunia wa kijamii nchini Kenya.
Wametoa wito wa kumalizwa kwa mizozo na kuazisha vita vipya dhidi ya umasikini.
Hii inakuja siku chache kabla ya mkutano wa dunia wa kiuchumi, mkusanyiko wa kila mwaka wa viongozi wa kisiasa na biashara mjini Davos, Uswisi.
Mkutano wa dunia wa kijamii ulianzishwa mwaka 2001 katika mkutano mbadala wa Davos.
Mkutano huo wa Nairobi ni wa kwanza kufanyika katika bara la Afrika na una lengo la kuelezea masuala kadha ya Afrika , ikiwa ni pamoja na HIV na ukimwi, kufutwa kwa madeni na utatuaji wa mizozo.
Kiasi cha watu 80,000 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo katika muda wa siku chache zijazo.