NAIROBI :Wanajeshi wa Ethiopia na Djibouti wakataliwa Somalia
27 Februari 2005Wababe wa vita wenye ushawishi nchini Somalia leo hii wamekataa uwezekano wa kuwekwa kwa wanajeshi kutoka Ethiopia na Djibouti kama sehemu ya kikosi cha eneo hilo kusaidia serikali ya mpito ya nchi hiyo kuweka mamlaka yake baada ya kurudi kutoka uhamishoni nchini Kenya.
Wamesema katika taarifa iliyotolewa Nairobi kufuatia mazungumzo ya jana usiku kwamba wanaidhinisha uwekaji wa vikosi vya kimataifa bila ya kuhusishwa kwa wanajeshi kutoka nchi jirani za Somalia .......Ethiopia na Djibouti.
Miongoni mwa wababe wa vita waliotia saini taarifa hiyo ni Hussein Mohamed Aidid ambaye pia ni naibu waziri mkuu, Mohamed Qanyare Afrah waziri wa usalama wa taifa na Musa Sudi Yalahow waziri wa biashara.
Vikaka hivyo vya vita pia wamesema wamekubali kusalimisha baadhi ya maeneo wanayoyadhibiti mjini Mogadishu kwa serikali ya mpito ambayo bado ingali imejichimbia nchini Kenya.